Msimamizi wa Uchaguzi Lamu kizimbani kwa kumpiga mgombea wa ubunge,Rishad Amana.

Angazo
Typography

 Msimamizi kura wa tume ya IEBC,Abdalla Chikophe amefunguliwa mashtaka ya kumpiga na kumjeruhi aliyekuwa mgombea kiti cha ubunge wa Lamu Magaharib  Rishad Amana.

Mnamo Agosti 10 katika kituo cha kuhesabu kura Mokowe Chikophe anadaiwa kumpiga na kumjeruhi Rishad Amana.

Msimamizi huyo wa kura  amekana mashataka hayo mbele ya Njeri Thuku. 

Na kesi hiyo itaskizwa Februari 22.

Na katika mahakama hiyo hiyo mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo amefikishwa katika mahakama Lamu kwa madai ya kigaidi.

Barisa Eleko Balola alitiwa mbaroni wiki iliyopita baada ya kupatikana na risasi kadhaa na sare za polisi.

Mshukiwa amekubali mashtaka hayo mbele ya hakimu Njeri Thuku.

Mahakama itatao hukumu  yake siku ya Ijumaa.