Viongzo wa kiislamu watakiwa kutengeneza mtaala mmoja wa mafunzo ya dini.

Angazo
Typography

Changamoto  imetolewa kwa taasisi za dini ya kislamu  kutengeza mtaala mmoja  utakaotumika kutoa mafunzo ya dini kote nchini.

Haya ni kwa mujibu wa Shekh Adam Hamisi aliyekuwa akizungumza  katika kongamano la aman eneo la Matuga Kaunti ya Kwale.

Ameutaja mtaala huo kama ambao utaweza kukabili mafunzo ya itikadi kali miongoni mwa vijana na kuwaepusha kujiunga na makundi ya kigaidi.

Adam amesema kuwa walimu wengi wa madhrasa kuwa hawana elimu ya kutosha katika kueleza wazi maswala ya utetezi wa dini ya kiislamu kupitia Jihad

Changamoto hii inajiri huku takwimu zikionyesha kuwa zaidi ya vijana 1000  kutoka kaunti ya Kwale walipokea mafunzo ya kigaidi nchini Somalia.