Mwanamume afariki baada ya kukanyagwa na gari moshi eneo la Changamwe.

Angazo
Typography

Mwanamume wa makamo ameaga dunia baada ya kukanyagwa na gari moshi usiku wa kuamkia leo eneo la Bogogoni eneo bunge la Changamwe.

Mwanamume huyo aliyetambulika kama Nyamawi alikanyagwa alipokuwa amelewa nyakati za saa tisa alfajiri.

Walioshuhudia mkasa huo wanasema mwendazake alizidiwa na pombe na akajilaza kwenye barabara ya reli,hali iliyosababisha kukanyagwa na treni hiyo.

Akithibitisha kisa hicho mama mtaa wa eneo hilo, Magret Nyangasi amesema kuwa hiyo sio ajali ya kwanza kufanyika mahali hapo. 

Aidha amewataka wenye biashara za pombe eneo hilo kuzifunga ili kuepeka maafa zaidi.

Wakati huo huo amewaomba wakazi kuwa makini wanapovuka katika njia ya gari moshi.