Wanafunzi watuzwa kwa kuswali swala ya Fajr bila kukosa kwa siku 40.

Angazo
Typography

Zaidi ya wanafunzi 50 wenye chini ya umri wa miaka 13 wametuzwa kwa kuswali swala ya Alfajiri mfululizo bila kukosa kwa siku 40 katika msikiti wa Al-Azhaar katika eneo la Guraya kaunti ya Mombasa.

Akiongea na meza yetu ya angazo mmoja wa walofanikisha hafla hiyo, Khalid Rubeiya ameitaja swala ya Alfajiri kama swala ngumu zaidi kati ya swala tano zilizofaradhishiwa.

Aidha amesema kuwa watafanya juhudi kuhakikisha kuwa vijana wengi wanaswali swala zote kama ilivyoa amrishwa na Mungu.

Amewataka vijana kujiepusha na makundi yenye itikadi kali na badala yake wabuni mbinu za kujinufaisha kwa kuambatana na sheria za dini.

Kwa upande wake mratili wa msikiti huo Yahya Ali Hassan,amesema kuwa sharti dini ya kiislam ipewe kipaumble,hasi shuleni na madrasa.