Mbunge ataka shisha kuhalalishwa kaunti ya Mombasa.

Angazo
Typography

Siku chache baada ya serikali kupiga marufuku utumizi wa Shisha,sasa mbunge mteule katika bunge la kaunti ya Mombasa Fatma Kushe,ametishia kuwasilisha mswada kwenye bunge la kaunti hiyo wa kuhalalisha biashara ya shisha hasa katika maeneo yaliyoidhinishwa na serikali ya kaunti hiyo.

Kushe amesema kila mkenya ana uhuru wa kujistarehesha na kileo anachotaka huku akiikosoa vikali hatua ya serikali kupiga marufuku utumiaji wa shisha.

Amesema wizara ya afya ya serikali ya kitaifa inapaswa kuheshimu sheria ya ugatuzi na kutambua kila serikali ya kaunti ina uhuru wa kuidhinisha sheria za kuwalinda wakazi wake.

Kauli yake inakinzana na za viongozi mbalimbali na wanaharakati wa kupambana na mihadarati katika kaunti kaunti ya Mombasa,ambao wanapongeza kuharamishwa kwa utumizi huo wa shisha.