Kura za ubunge wa Lamu Magharib zahesabiwa upya.

Angazo
Typography

Kura za kiti cha ubunge wa Lamu magharibi zinahesabiwa tena upya katika kituo kikuu cha IEBC cha  Mokowe baada ya agizo la mahakama ya Malindi

Hii ni baada ya mmoja mgombea kiti hicho cha Lamu Magharib, Rishad Amana kuwasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa mbunge Stanley Muthama.

Maafisa wa usalama wamepiga kambi kwenye kituo hicho ili kuweka usalama wa kutosha wakati zaozi hilo likiendelea.

Naibu msajili wa mahakama ya Malindi,Waandia Nyamu pamoja na wangalizi kutoka pande zote wanashuhudia kuhesabiwa kwa kura hizo.

Agizo la kuhesabiwa upya kwa kura hizo lilitolewa na jaji Weldon Korir mwezi uliopita katika mahakama ya Malindi.

More to follow........