Jaji kuamua iwapo atajiondoa kwenye kesi ya kupinga ushindi wa Joho.

Angazo
Typography

Uamuzi wa iwapo jaji Lydia Achode anafaa kijutoa kwenye kesi ya kupinga ushindi wa gavana wa Mombasa Hassan Joho utaolewa Ijumaa wiki ijayo.

Hii ni baada ya aliyekuwa seneta wa Mombasa Hassan Sarai kumtaka jaji huyo kujiondoa kwenye kesi hiyo kwa madai kuwa anapendelea upande wa Joho pekee.

Sarai  kupitia wakili wake Yusuf Abubakar,anasema kuwa hakuna usawa katika kusikilizwa kesi hiyo tangu ianze rasmi.

Wakili Abubakar ameongeza kuwa sharti jaji huyo ajiondoe ili jaji mkuu nchini David Maraga aweze kuchagua jaji mwengine atakayesikiliza kesi hiyo kwa haki,uwazi na usawa.

Kwa upande wake Joho,kupitia wakili wake Mohammed Balala amepinga ombi la Sarai na kulitaja kama lililopitwa na wakati ikizingatiwa kesi hiyo inaelekea kukamilika.

Aidha,wakili Balala ameitaja hatua ya Sarai kama anahisi kushindwa kwenye kesi hiyo.

Balala amesema kuwa itakuwa vigumu kwa jaji mkuu kuweza kuchagua jaji mwengine kuweza kusikiliza kesi hiyo kwa siku 30 pekee ambazo zimebakia kwa sasa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

Kulingana na sheria  ni kwamba kesi za uchaguzi zinaafa kusikilizwa na kutamatika kwa muda wa miezi sita pekee kuanzia siku ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi.