25
Sun, Feb

Raia auwawa baada ya Al-Shabaab kushambulia msafara wa mabasi Lamu

Angazo
Typography

Mwanamke mmoja ameaga dunia huku maafisa watano wakijeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa Al-Shabaab katika kaunti ya Lamu mwendo wa tano asubuhi ya leo.

 

Wanamgambo hao wameshambulia magari ya maafisa wa usalama waliokuwa wakisindikiza msafara wa mabasi ya abiria  yaliyokuwa yakitoka Lamu kuelekea Mombasa katika barabara ya  Mombasa-lAMU katika eneo la Nyongoro huko Lamu.

Kwenye makabiliano kati ya maafisa wa polisi na wanamgambo hao, maafisa kadhaa wa usalama wamejeruhiwa huku raia mmoja  aliyekuwa ndani ya gari la maafisa hao ameaga dunia.

Katika shambulizi hilo magari mawili ya maafisa wa usalama yamechomwa moto na wanamgambo hao.

Aidha msafara huo wa mabasi umeweza kusindikizwa na maafisa wengine kuendelea na safari.

Kamishna wa kaunti ya Lamu Gilbert Kitiyo amethibitisha tukio hilo na kwa sasa operesheni inaendelea kuwasaka magaidi hao na afisa mmoja aliyekuwa wakati wa tukio hilo.