25
Sun, Feb

Bunge la kitaifa kuregelea vikao vyake leo.

Angazo
Typography

Bunge linatarajiwa kuregelea vikao vyake  hii  leo baada ya likizo ya majuma mawili. 

Shughuli kuu ni kujadili  na kuidhinisha  watu walioteuliwa kuhudumu katika baraza la mawaziri. 

Kamati ya bunge kuhusu uteuzi itawasilisha ripoti yake baada ya kuwapiga msasa tisa hao walioteuiliwa kuhudumu katika baraza la mawaziri Alhamisi na Ijumaa iliyopita.   

Walioteuliwa  ni John Munyes wa wizara ya Mafuta ya Petroli na Madini, Monica Juma wa Mashauri ya Kigeni,  Farida Karoney  wa ardhi na Nyumba,  Peter Munya wa Maswala ya Afrika Mashariki na Ustawi wa  Miradi ya miundo msingi na  Profesa Margaret Kobia wa Utumishi wa Umma, Vijana na Jinsia. 

Wengine walioteuliwa ni  Keriako Tobiko wa Mazingira na Misitu,  Simon Chelugui wa Maji na Usafi, Ukur Yatani wa Leba na Huduma za Jamii  na Rashid Achesa  wa Michezo na Turathi. 

Aidha mjadala mkali kuhusiana na uteuzi wa 9 hao unatazamiwa kusheheni mkao huo.

Ni mkao ambao unatarajiwa kushuhudia cheche pia kutoka kwa wabunge wa upinzani wakilalamikia kupokonywa walinzi na hata umiliki wa bunduki.