25
Sun, Feb

Leo ni siku ya Radio Ulimwenguni.

Angazo
Typography

Leo ni siku ya radio ulimwenguni.

Watangazaji na wanahabari wa Radio mbalimbali humu nchini pia wamejiunga na wenzao ulimwenguni kusherehekea siku hii kwa njia mbalimbali hasa katika mitandao ya kijamii.

Ambapo mashabiki pia wameweza kuwalimbikizia sifa kochokocho watangazaji wanaowaenzi.

Tangu kuanza kwa Radio ulimwenguni takriban miaka 98 sasa, umuhimu na sifa zake zimeweza kuenea kote duniani kulinganana na mafunzo na taarifa zinazochipuka kila uchao. 

Wananchi kutoka sehemu mbalimbali hapa jijini Mombasa wameweza kuzungumza kuhusu  upeperushaji wa  wa taarifa kupitia njia ya radio.

Kutokana na ukuaji  wa vituo vingi vya radio nchini na kote ulimwenguni, umuhimu wake na nafasi katika maisha ya watu pia umeongezeka mno. 

Hapa jijini Mombasa wafanyibiashara na wananchi wa kawaida kwa jumla wameusifu mfumo huu wa upeperushaji wa matangazo na taarifa.

Baadhi yao wanasema kwamba Radio imechangia pakubwa katika ukuaji wa amani nchini sawia na kutoa taarifa tendeti kipindi cha siasa kilichokamilika mwishoni mwa mwaka jana, sawia na sherehe ya kuapishwa kwa kiongozi wa NASA Raila Odinga mwishoni mwa mwezi jana.

Idadi kubwa ya watu hata hivyo wanasema hawana muda wa kusikiliza Radio lakini iwapo wanapata nafasi basi wao husikiliza taarifa na burudani.