25
Sun, Feb

Mawakili wa Mombasa waionya serikali dhidi ya kikiuka katiba.

Angazo
Typography

Chama cha mawakili tawi la Mombasa kimeitaka serikali kuheshimu katiba na kukoma kupuuza maagizo ya mahakama.

Akizungumza na wanahabari katika jengo la mahakama ya Mombasa, mwenyekiti wa chama hicho Mombasa Mathew Nyabena amesema sharti viongozi wakuu serikalini kuheshimu katiba ili kuwa mfano kwa wananchi.

Nyabena ameongeza kuwa siku ya Alhamisi wataandaa maandamano kulaani visa vya ukiukaji wa maagizo ya mahakama.

Kwa upande wake seneta wa Mombasa ambaye pia ni wakili Mohammed Faki ameilamu serikali kwa kuwa mstari wa mbele kuvunja sheria za taifa.

Naye wakili Jerad Magolo amesema wataelekea mahakamani kupinga ukiukaji wa sheria pindi tu katiba inapokiukwa.

Kauli zao zinajiri baada ya Inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinet na mkuu wa idara ya upelelezi George Kinoti kudinda kumwasilisha mahakamani na kumuachilia huru mwanasiasa wa upinzani Miguna Miguna na badala yake kumsafirisha hadi nchini Canada.