25
Sun, Feb

Mshukiwa wa wizi wa pesa apata kichapo cha Mbwa Malindi

Angazo
Typography

Shughuli za kawaida zilitatizika katikati ya mji wa Malindi baada ya wananchi kumvamia na kumpa kipigo cha mbwa teja aliyedaiwa kuiba pesa.

Teja huyo ambaye pia anahudumu kama manamba wa gari za kuelekea Gongoni, anadaiwa kuiba shilingi elfu tano akiwa na manamba mwenzake ambaye alifaulu kutoroka.

Wizi huo ulitokea pale mwenye duka alipomtuma mmoja wa manamba kuenda kudai shilingi elfu tano pesa ya biashara, lakini manamba huyo hakurudi baada ya kulipwa pesa hizo na baadae akashirikiana na mwenzake  kugawanya pesa hizo.

Licha ya teja huyo kuwarai waliokuwa wakimpiga kwamba sio yeye ameiba, rai hiyo iliangukia patupu kwani waliendelea kumpiga makonde na mateke na kumlowesha damu.

Katika harakati hizo, teja huyo alipatikana na shilingi mia nane katika mfuko wake wa suruali na kusema wakati akifukuzwa alipoteza shilingi elfu moja lakini akakana kwamba pesa hiyo ni ya wizi huku akisema ataenda polisi kushtaki.