25
Sun, Feb

Kenya kushuhudia mvua kiwango cha kawaida na zaidi ndani ya miezi mitatu ijayo.

Angazo
Typography

Huenda sehemu za mashariki mwa Kenya zikashuhudia mvua kiwango cha kawaida na zaidi ndani ya miezi mitatu ijayo ambayo huenda ikasababisha mafuriko.

Akisoma ripoti ya pamoja ya nchi wanachama wa IGAD wakati wa kufungwa kwa kongamano la siku mbili katika hoteli moja hapa Mombasa mwelekezi katika idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Peter Ambenje amesema kuwa sehemu nyengine zinazotarajia mvua kama hiyo ni mashariki mwa Ethiopia na sehemu nyingi za Somalia.

Ameongeza kuwa kwa sasa kuna ishara za ukame maarufu kama La Nina lakini bado inafanyiwa uchunguzi na baada ya miezi mitatu ripoti kamili itatolewa.

Baada ya kutolewa kwa ripoti hiyo ya pamoja kwa nchi 11 za IGAD sasa idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini inatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusu mvua ya mwezi Machi hadi Aprili nchini siku ya Jumatatu baada ya kuijadili zaidi ripoti hiyo.