25
Sun, Feb

Mwanasheria mkuu nchini Githu Muigai ajiuzulu.

Angazo
Typography

Mkuu wa sheria Githu Muigai amejiuzulu baada ya kuhudumu katika wadhfa huo kwa kipindi cha miaka sita na nusu.

Rais Uhuru Kenyatta katika taarifa yake amethibitisha kupokea  barua ya kujiuzulu kwa Muigai na kumteua  rais wa mahakama ya rufaa jaji Paul Kihara Kariuki  kuwa kaimu  mkuu wa sheria.

Aidha aliyekuwa mmoja wa mawakili wa rais wakati wa kesi yake katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC Kennedy Ogeto ameteuliwa kuwa mwansheria mkuu wa serikali baada ya Njee Muturi aliyekuwa akishikilia wadhfa huo kuteuliwa kama naibu mkuu wa wafanyikazi ambapo atakuwa naibu wa Nzioka Waita.

Abdikadir Mohammed aliyekuwa mshauri wa rais kuhusu masuala ya katiba na sheria ameteuliwa kuwa balozi wa Kenya nchini Korea Kusini.