Asilimia 33 ya wakenya wanamtaka Raila astaafu katika siasa

Siasa
Typography

Asilimia 27 wanasema aendelee kuwa katika fani hiyo ila asiwanie urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Aidha asilimia 34 ya waliohojiwa wanataka Raila asalie katika siasa na pia kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Vile vile utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 58 ya wakenya hawana imani na tume ya uchaguzi nchini IEBC kuendesha uchaguzi mkuu ujao.

Utafiti huo uliofanywa kwa siku kumi mwishoni mwa mwezi Machi na mapema April unaonyesha kuwa kati ya watu 1, 964 ya waliohojiwa asilimia 42 wako na imani na tume hiyo.

Wengi wa walio na imani na tume ya IEBC ni wafuasi wa mrengo wa Jubilee wakiwakilisha kwa asilimia 61 na wale Wa mrengo wa CORD wakiwa asilimia 21.

Zaidi imeonyesha kuwa asilimia 35 wanaoishi mijini wanaiunga mkono tume hiyo ikilinganishwa na asilimia 46 ya wakenya wanaoishi mashambani.