CORD yamtetea Kalonzo Musyoka

Siasa
Typography

Kiongozi wa walio wachache katika bunge la kitaifa Francis Nyenze na Seneta Maalum Judith Sijeny,  wakizungumza jijini Nairobi wametaja madai yanayoendelezwa na Jubilee kuwa Kalonzo alinyakua shamba la Yatta hayana msingi na kuwa kipande hicho cha ardhi alikinunua kwa njia ya halali kutoka kwa mfanyabiashara Janet Chirchir na Kampuni ya Betracal miaka ya 90.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya Waziri wa Ardhi aliyesimamishwa kazi Charity Ngilu kumtetea Kalonzo, akisema kuwa ardhi hiyo aliipata kwa njia ya halali kwa ushahidi wa stakabadhi zilizopo katika wizara aliyokua akiisimamia.