Waliopoteza viti vyao CORD wazidi kujiunga na JUBILEE

Siasa
Typography

Hii nii baada ya mwanachama mwengine kutoka  chama cha Wiper Fahad Kassim kuhama  mrengo huo  na kujiunga na chama cha JAP.

Fahad ambaye aliwania kiti cha ubunge eneo la Kisauni katika uchaguzi mkuu uliiopita kupitia tiketi ya chama cha Wiper amesema amechukua mwelekeo  huo kutokana na utendakazi wa rais Uhuru Kenyatta kwa watu wa Pwani ambaye ndio kinara wa muungano huo huku akikashifu muungano wa CORD hapa Pwani kwa madai  ya kutoonyesha maendeleo yoyote.

Mwenyekiti wa chama cha TNA kaunti  ya Mombasa Matano Chengo ameonya kuwa  kwa sasa chama cha JAP kinapanga kuteka eneo  la Pwani ambayo ndio  ngome kuu ya muungano wa CORD.

Akihutubia wafuasi wao katika hoteli moja hapa Mombasa kwenye hafla ya kumkaribisha ,amedai kuwa muungano wa upinzani umekosa mwelekeo akitolea mfano rabsha zilizoshuhudiwa katika kaunti ya Migori katika uchaguzi wa mashinani wa chama cha ODM ambapo watu watatu waliuwawa na wengine kujeruhiwa.

Haya  yanajiri siku chache  baada ya ziara ya rais  Uhuru Kenyatta hapa Mombasa ambapo alikutana na wanachama wa  muungano wake katika ikulu ya rais ishara  ya kuimarisha umaarufu  wa Jubilee hapa Pwani ambayo ndio ngome kuu ya upinzani,ikiwa  ni miezi kadhaa baada ya wanachama wengine wa CORD Suleiman Shahbal wa Wiper na Ramadhan Kajembe wa ODM  kuhama muungano huo na kujiunga na JAP.

LIVE RadioRahma via the App