Raila asema serikali inatumia hila kusambaratisha CORD

Siasa
Typography

Amesema swala la kutaka kutoa jina la seneta Moses Wetangula katika sajili la wapiga kura ni njama ya kuwayumbisha kisiasa na kusambaratisha umoja wa muungano huo.

Aidha amemtetea aliyekuwa meya wa Nairobi George Aladwa akisema kwamba hana hatia ila aliwaonya tu wale walio na nia ya kuiba kura mwaka 2017 huku akizikashifu mahakama kwa kutumiwa vibaya na serikali ya JUBILEE

Wakati huo huo ameikashifu serikali kwa kuchangia kudorora kwa uchumi wa taifa kwa kufuja pesa za umma kwa njia isioeleweka na kukosa kupiga vita ufisadi.