Chama chengine cha JUBILEE kuundwa

Siasa
Typography

Akizungumza katika mkutano wa chama cha JAP mwenyekiti wa kamati iliyoundwa kuja na chama kimoja cha muungano wa Jubilee Noah Wekesa amesema wamekubaliana kuunda kamati tisa ambazo zitahakikisha kuwa vyama vyote ndani ya muungano wa Jubilee vinajiunga na kuwa chama kimoja.

JAP imekuwa ikimpigia kampeni rais Uhuru Kenyatta kuchaguliwa tena mwaka 2017 lakini baadhi ya vyama kikiwemo chama cha APK cha seneta wa kaunti ya Meru Kiraitu Murungi vimekuwa vikisitasita kujiunga na JAB kwa sababu hawakushauriwa.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wenyekiti na makatibu wakuu wa vyama vya TNA, URP, APK, New Ford Kenya na JAP.