Ababu ajipata mashakani Mombasa baada ya vijana kumvamia na kumwita msaliti

Siasa
Typography

Vijana hao zaidi ya 30 walimtaka Ababu kueleza sababu za kukihama chama cha ODM huku wakimtaja kama msaliti kwa kiongozi wa chama hicho Raila Odinga.

Ilichukua juhudi za katibu mtendaji wa chama hicho Peter Ole Musei kuwatuliza vijana hao waliokuwa na ghadhabu.

Kwenye hotuba yake alipokua katika ibada ya kanisa hilo, Namwamba amesema lengo la chama cha Labour  ni kuhakikisha mwanachi wa mashinani aliyesahaulika kwa muda mrefu anapata haki na usawa  kimaendeleo.

Mbunge huyo pia amekashifu serekali Jubilee kwa kutowajibikia  matatizo yanayowakumba wananchi wake, huku akiwaomba viongozi wa maeneo yaliyoathirika na baa la njaa kuchukua hatua za dharura ili kusoluhisha tatizo hilo.

Namwamba ameeleezea kuwa endapo hawatafaulu  kuchagua kinara wa chama cha LPK wataunga mkono  mgombezi wa uraisi aidha wa Cord Ama Jubilee lakini kuambatana na utendaji kazi na  makubaliano ndani ya vyama hivyo.

Ababu  yuko katika ziara hapa Pwani kukitafuta umaarufu na wafuasi chama hicho.