Mashahidi saba wa Sarai, hawatashiriki kwenye kesi ya kupinga ushindi wa Joho.

Siasa
Typography

 Mashahidi saba kati ya 19 wa aliyekuwa seneta wa Mombasa Hassan Sarai wameondolewa kwenye kesi ya kupinga ushindi wa gavana wa Mombasa Hassan Joho.

Saba hao hawatashiriki kwenye kesi hiyo baada ya kubainika kuwa ushahidi wao ni wa uvumi wala si wa ukweli.

Wakati huo huo jaji Lydia Achode amesema kuwa mahakama haitazingatia ushahidi ambao haumbatani na kanuni za sheria za uchaguzi kwa mujibu wa katiba.

Aidha,ameongeza kuwa hatazingatia Fomu za matokeo ambazo hazina muhuri wa tume ya uchaguzi zilizowasilishwa na Sarai.

Haya yanajiri baada ya mawakili wa Joho ,wakiongozwa na Denis Musota na Mohammed Balala kuwasilisha ombi la kutaka kutupiliwa mbali kwa kesi hiyo kwa kusema kuwa nakala zilizowasilshwa hazina muhuri wa Iebc.

Naye Jaji Achode amesema kuwa kesi hiyo itaendelea lakini akatoa onyo kuwa hatazingatia ushahidi wowote wa uvumi utakao wasilishwa mbele yake.