Raila asema tume ya kukabiliana na ufisadi inajivuta kwa walio ‘kula kuku’

Siasa
Typography

Raila amesema maafisa wa tume hiyo wanafaa kuchukua taarifa juu ya kashfa hiyo kutoka kwa kitengo cha kukabiliana na ubaridhifu mkuu kutoka Uingereza waliofanya uchunguzi wa kashfa hiyo.

Ameeleza kuwa haina haja kwa tume hiyo kusema inatafuta ushahidi ambao tayari upo huku akidai serikali inawaficha wahusika hao.

Wakuu wawili wa kampuni ya uchapishaji ya Smith na Ouzman nchini uingereza wamefungwa kwa kuwahonga maafisa wa tume ya uchaguzi nchini IEBC ili kupata zabuni ya kutengeza makaratasi ya kupigia kura.