Raila kukutana na wabunge kuiokoa hazina ya CDF

Siasa
Typography

Mikutano sawa na hiyo pia itafanywa na maseneta na magavana kama ilivyoagiza mahakama kujumuishwa kwao katika kuundwa na utekelezwaji wa hazina hiyo kulingana na katiba ya sasa. 

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Raila amesema ameagiza kamati ya wataalamu ya Okoa Kenya kubuni marekebisho ya sheria yatakayokuwa chanzo cha kujumuishwa kwa hazina hiyo katika katiba kupitia kura ya maoni.

Zaidi Raila amesema miongoni mwa maswala yaliyobuniwa na kamati hiyo ya wataalamu ni kwamba kutakuwa na hazina ya maendeleo kwa kika wadi nchini.