Wetangula atangaza kuwania Urais

Siasa
Typography

Wiki mbili baada ya kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua kutangaza kuwania tena kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao, seneta wa Bungoma Moses Wetangula naye pia ametangaza kuwania kiti hicho. 

Wiki mbili baada ya kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua kutangaza kuwania tena kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao, seneta wa Bungoma Moses Wetangula naye pia ametangaza kuwania kiti hicho. 

Akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa chama cha Ford Kenya huko Gillgil, Wetangula amesema yuko tayari kwa kinyang`anyiro hicho. 

Zaidi amesema yeye ndiye anayefaa kuongoza taifa hili ili kuondoa uongozi mbaya ambao umedumu hadi sasa.

Wetangula amesema swala la kukabiliana na ufisadi litakuwa agenda yake kubwa katika kampeni sawa na swala la usalama.

LIVE RadioRahma via the App