Msichana aendelea kumea uvimbe wa maajabu shingoni huko Magongo

Taarifa Za Kaunti
Typography

Msichana mwenye umri wa miaka 22 kutoka eneo la Bomu, Magongo, anakabiliwa na wakati mgumu kutokana na maumivu ya uvimbe mkubwa unaoendelea kumea mwilini mwake. 

Msichana mwenye umri wa miaka 22 kutoka eneo la Bomu, Magongo, anakabiliwa na wakati mgumu kutokana na maumivu ya uvimbe mkubwa unaoendelea kumea mwilini mwake. 

Kulingana na mamake mdogo, Mariam Kombo, uvimbe huo unaoendelea kukua shingoni ukielekea mgongoni unampa mwanadada huyo maumivu makali kichwani na kumfanya kushindwa kutembea. 

Uvimbe huo ulianza kama baku refu kutoka kichwani hadi mgongoni na alipomaliza darasa la nane ndio baku hilo likaanza  kuvimba japo uvimbe huo ilikuwa hauumi. 

Kwa wakati huo daktari alisema kunahitajika upasuaji ambao ulikuwa hakuna uhakika wa kupona hivyo basi familia kuamua kutofanyiwa upasuaji kwa sababu ilikuwa haumwi.

Mariam anasema kwa muda wa mwezi mmoja sasa uvimbe huo umekuwa mkubwa sana na unaendelea kukua. 

Mwanahabri wetu hakuweza kuzungumza na msichana huyo kwa sababu ya maumivu lakini anaeleza kuwa anahisi kama mzigo mzito mgongoni. 

Hata hivyo juhudi zao za kuhakikisha amepata matibabu zinatatizika kutokana na uhaba wa fedha hivyo kuhitaji jamii kuwasaidia. 

Aidha Mariam ameeleza meza yetu ya Angazo kwamba wanahitajika kwenda hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi.

Account name: Mariam Abdalla Kombo

Account number: 0101071801

Bank Name: Gulf African Bank

Branch: Bombolulu branch

------------------------

Safaricom Paybill Number: 985050