Makala Maalum - Kujipiga Punyeto (Masturbation)

Makala Maalum
Typography

Daktar Ali Omar ni mtaalmu wa akili anafafanua maana ya mastabation au kupiga punyeto. 

“Masturbation maana yake ni kujishika nafsi  yako kiwa ni mwanamke au kushika dhakari yako kiwa ni mwanamume ukanza kuipapasa ili mpaka ufikie ile kileleni - sexual climax”

Nimezungumza na kijana wa miaka 20 Rona Suleiman amabaye hadi sasa anaendeleza kufanya punyeto ananieleze vipi alijipata kwenye kitendo hicho. 

“sababu ambayo inanifanya nifanye punyeto ni kuangalia pornographs na nlikua naziangalia kwenye tv saa nyingine kwenye simu”

Je Rona uhisi vipi akikosa kufanya masturbation? 

“Kusema kweli uwa sisikii vizuri kwa sababu ni mazoea yangu na nilianza kitambo sana yaani saa hii niko na mwaka wa pili tangu nianze hivyo”

Je kuna uwezeakano wakufanya mapenzi kiholela na wasichana iwapo hisia zinampanda anapotazaama video za ngono.

“Kusema ukweli kwanza kitu kilinifanya niangalie hivyo nilikuwa sipati wasichana na nikiangalia kwenye simu vile pornographs zinafanywa ili nijifanye mwenyewe tu”

Nilivulia njuga swala hili ili kuweka wazi madhara ya masturbation kwa vijana.

Daktari Omar Ally, hapa anaelezea  sababu kuu inayochangia masturbation kwa vijana.

“Sasa saa nyingine watu  namna ile uwa wana maradhi, wana ugonjwa huwa twasema wanazo zile sexual disorders na sexual disorders ni nyingi kuna wengine mtu  mpaka akae aangalie picha akishangalia picha vile za wanawake au za watu wanafanya ngono au kitu namna hii ndio na yeye upata nguvu sasa yule huenda alafu akafanya hiyo masturbation naye akapata gratification, sasa hizi hizi twaziita sex sexual divients manake ni kuwa mpaka upate kitu chengine chochote cha kukufanya utambue kuwa you have to have this gratification hasa zile tunaita sexual disorders”

Jambo lolote halikosi wafuasi je ni kinanai wanajihusisha na upigaji punyeto kwa hasa.

“sasa kuna na watu wengine Mungu mwenyewe amewaumba kuwa ni watu wako na haya hawezi kumfuata msichana ama mvulana kujamiiana naye ili kujitosheleza sasa hawa ndio uwa wanaendelea na tabia ile anajifungia mahali na kujibana ili ajitosheleze,

katika hizi sexual disorders nyengine, watu wengine hufanya kitendo hiki kitendo hiki mbele za watu au mbele za watu  wa opposite sex,

nilipokuwa mdogo tulikuwa tukimuona bwana mmoja akiona watoto wa kike ujifungua sehemu za siri kisha akaakanza kufanya kitendo hiki, sasa wale tuna waita exhibinist au watu ambao kwamba wanapenda kujiexpose kwa the opposite sex.

Kuna waitwao sedist hawa hawapati ile sexual sertisfaction bila ya kuwaumiza watu wengine wanawapiga watu  wengine, kuna wengine wanaitwa masochist au masochism. masochism ni kuwa mtu awe anapata dharubu ndio anafika kileleni” 

Je wanaofanya punyeto wanajua madhara yake huyu hapa kijana anazungumza nami. 

Rona…Paka sasa mimi sijajua madhara yake ndio maana naendelea tu kufanya. 

Kila kitu hakikosi madhara japo wengi hawatambui haya,Je wanaofanya masturbation upata madhara gani , daktari Omar Ally anaelezea. 

“Madhara ya kufanya sana  jambo hili ni roho yako inaendelea kuona kuwa hiyo ndio njia pekee ya kujitosheleza kingono na hautajua njia nyengine nah ii inaathiri sana familia.

Madhara yake sana ni unaweza kujichubua lakini ile long term ni ile utakuwa si mtu wa kikawaida. Madhara yake sana makubwa ambayo kwamba watu wanayohofia sana nikuwa akili yako sasa itakuwa haina namna nyingine isipokuwa kufanya kitendo kama kile ambacho kwamba si kitendo cha kisawasawa kabisa”

Kila kitu hakikosi mwisho wake je Rona yuko tayari kuacha kufanya masturbation au kupiga punyeto. 

"Kusema kweli kuacha saa ii ni vigumu sana kwa sababu yaani nikikosa kufanya kwa siku huwa si siki vizuri."     

Ili kuepukana na tatizo hili Daktari OMAR ana suluhu kwa wapigaji punyeto. 

"Ni uzuri aende kwa wale tunawaita behaviourist au behavior therapist ambao kwamba watamtibu na matibabu yake si ya dawa sana ni matibabu ya kumfanya mtu awache tabia moja aingie tabia nyingine."

Nilitaka kujaua dini ya kiislamu inaangazia vipi swala la upigaji punyeto Ustadh Shabban Abdu Musa ni mwenyekiti wa maulama na maimamu nchini KAULI,a nafafanua swala hili.

“katika jambo ambalo uislamu umelikemea ni kujipiga punyeto yaani kutumia mkono katika kujitoza maani ni jambo ambalo kwamba ni haramu katika uislamu, uharamu wake mtume [SWA]katika hadhithi swahihi asema mwenyezimungu amemtoa katika rehema yake maanake mwenyezimungu amemlaani Yule ambae mwenye kuoa mkono wake,yani akafanya mkono wake ndio anajitumia katika sehemu zake za siri kujitoza mani.

Kitendo cha kujipiga punyeto ni haramu katika sheria za uislamu na mtu iwapo atafanya kitendo kile yaupat mdhambi na laana kwa mwenyezimungu

Je kijana wa kiislamu atajiepusha vipi na upigaji punyeto, Ustadh Shabban anaelezea.

Ni kutoangalia filimu za wanawake walio uchi, za haramu kutokwenda pengine katika fuoni za bahari kuwatizama wanawake ambao wanakwenda uchi

 

- Makala yametayarishwa na Athman Luchi.