Biashara ya nyama yakosa soko Mombasa

Uchumi/Biashara
Typography

Biashara ya nyama masokoni imedorora kwa kiwango kikubwa kwa siku ya tatu sasa kufuatia sherehe ya idul adhhaa.

Biashara ya nyama masokoni imedorora kwa kiwango kikubwa kwa siku ya tatu sasa kufuatia sherehe ya idul adhhaa.

Hali hii imetokana na sheria ya dini inayotekelezwa katika siku hiyo ya kuchinja.

Akizungumza na mwanahabari wetu mwenyekiti wa soko la nyama la market Ali Aden amesema kuwa wauzaji wamepoteza wateja kutokana na kuwa wateja wengi wa nyama ni waislamu hali iliowalazimu kupunguza kiwango cha nyama wanacho chukua kichinjioni.

Hata hivyo wanatarajia hali hiyo kubadilika kuanzia hapo kesho.