25
Sun, Feb

Posta yazindua M-Post pwani

Uchumi/Biashara
Typography

Akizungumza wakati wa uzunduzi huo mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Dan Kagwe amesema kuwa huduma hiyo ni katika hali ya kuboresha huduma zao sambamba na kuvutia wateja zaidi kupata huduma hizo.

Aidha huduma hiyo ya M POST inalenga kuongeza idadi ya wateja wanaotumia visanduku vya posta 6,50000 hadi wateja milioni 30.

Kupanuka kwa huduma hiyo aidha kutatoa nafasi zaidi za ajira kwa wakenya ikizingatiwa kuwa wateja watakua na uhuru wakuchagua wanakotaka kupokea mizigo yao au barua hali itakayolazimu kuweko kwa wahudumu zaidi ili kufikisha huduma hizo mashinani.

Vile vile wateja watakaotumia huduma hiyo watalipa ada ya shilingi 300 kwa mwaka kinyume na shilingi 2300 zinazolipwa kwa mwaka kwa wanaotumia visanduku vya posta.

Huduma hiyo imezinduliwa kwa mara ya kwanza katika ukanda wa pwani huku ikiwa ni uzinduzi wa pili nchini baada ya kuzinduliwa jijini Nairobi.