Bei ya Mafuta kupanda kote Ulimwenguni

Uchumi/Biashara
Typography

Bei ya mafuta duniani imeanza kupanda baada ya muungano wa mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi, Opec, kukubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minane.

Bei ya mafuta duniani imeanza kupanda baada ya muungano wa mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi, Opec, kukubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minane.

Habari za kufikiwa kwa makubaliano hayo zimesababisha kupanda kwa bei ya mafuta ghafi kwa karibu asilimia 6.

Wanachama wa Opec wamekuwa wakilaumiana kusababisha mdororo wa bei ya mafuta kutokana na wao kushindwa kuchukua msimamo mmoja wa kudhibiti bei.

Wanachama wa Opec wamekuwa wakikutana Algeria.

Mafuta ghafi ya Brent, yanayotumiwa kama kigezo cha mafuta kimataifa, yalipanda bei na kufikia karibu asilimia 6 hadi $49 kila pipa baada ya tangazo hilo kutolewa.

Mawaziri wa mafuta wa nchi wanachama wamesema maelezo ya kina kuhusu mwafaka wa sasa yatajadiliwa kwenye mkutano mwingine Novemba.