25
Sun, Feb

Mradi wa alovera wanufaisha wakaazi Ganze

Uchumi/Biashara
Typography

Kadzitu Karisa mmoja wa wakazi hao amesema kuwa mmea wa alovera humea mwituni na wamekuwa wakiutumia kama dawa ya kuponya vidonda miongoni mwa maradhi mengine.

Kulingana na Kadzitu  bidhaa hiyo imewavutia madalali mbalimbali kutoka hapa mjini Mombasa ambao huuza kwa wataalamu wa dawa ili kutengenezwa dawa mbalimbali.

Hata hivyo wanabishara hao wamesema kuwa maji hayo ya alovera huuzwa kwa shilingi mia sita kwa mtungi wa lita tano jambo walilolitaja kama kudhulumiwa.

Naye mtaalamu wa uwekezaji katika kaunti ya Kilifi Maitha Masha amesema kuwa iwapo wakazi hao watapewa mbinu mpya za kukamua maji hayo kutoka kwa mmea wa alovera huenda maisha yao yakabadilika pakubwa.