25
Sun, Feb

Mbunge ataka wakulima wa mmea wa Mnazi kufidiwa.

Uchumi/Biashara
Typography

Mbunge wa Kilifi Kazkazini Owen Baya amepeleka mswada bungeni kuona kama wakulima wa mmea wa mnazi wanaweza kufidiwa.

 Hatua yake inajiri baada ya wakulima wengi kupoteza mimea yao ya minazi kutokana na kiangazi cha muda mrefu.

Kulingana na Owen Mswada huo unaitaka serikali kuwapa fidia ya shilingi milioni mia tatu wakulima hao ili waweze kupanda aina ya mnazi wa kisasa.

Kaunti ya Kilifi ni miongoni mwa kaunti ambazo zinakuza kwa wingi mmea wa mnazi na wananchi wengi wamekuwa wakiutegema katika kuboresha maisha yao.