25
Sun, Feb

Sekta ya bodaboda yaimarika licha ya kukumbwa na changamoto nyingi.

Uchumi/Biashara
Typography

Licha ya changamoto zinazokumba biashara ya bodaboda katika maeneo mbalimbali humu nchini sekta hiyo imeonekana kuimarika zaidi.

Katika uchunguzi uliofanywa na meza yetu ya biashara tumebaini kuwa vijana wengi hasa wanaomaliza darasa la nane na wale wanaoacha shule mapema hujihusisha na biashara hizo hasa katika maeneo ya vijijini kabla kwenda mijini kufanya biashara hiyo.

Hata hivyo asilimia kubwa wanaojihusisha na udereva wa pikipiki hizo huwa hawajapata mafunzo yoyote ya udereva.

Tulizungumza na Karisa Hamisi mmoja wa wahudumu hao ambae ameeleza kuwa vijana hufunzana wenywe kwa wenywe hasa katika sehemu zisizo na msongamonao kisha kuanza kupewa pikipiki amambapo hubeba katika sehemu za karibu marufu ‘squad ‘na wanapopata ujuzi zaidi ndipo ujiunga kikamilifiu katika kazi hiyo.

Vile vile tumebaini kuwa wengi wa vijana wanapokua na ujuzi hujinunulia pikipiki zao kwa njia ya mkopo jambo linalozidi kuimarisha sekta hiyo.