25
Sun, Feb

Bunge la EALA laanza kukagua miradi ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

Uchumi/Biashara
Typography

Wabunge wa bunge la Afrika Mashariki EALA wameanza rasmi ukaguzi wa miradi walioafikiana katika mataifa ya jumuiya  ya Afrika Mashariki ili kurahisisha biashara katika mataifa hayo.

Akizungumza na wanahabari mbunge wa Uganda anaewaskilisha spika wa bunge hilo Mathius Kasamba amesema ziara hiyo ya ukaguzi iliyoanza hii leo inalenga kuwafahamisha wananchi wa mataifa wanachama jukumu la bunge hilo katika kuhakikisha malengo yake yanatimia.

 Kasamba amesema kwa ushirikiano wanapanga kumaliza changamoto zinazokabili miradi hiyo pamoja na kuondoa vizingiti vya kibiashara vinavyoshuhudiwa ndani ya mataifa hayo wanachama.

 Wakati huo huo ameipongeza halmashauri ya bandari ya Mombasa kwa kuboresha miundo msingi ambapo ameeleza kuwa umeboresha utendakazi katika usafirishaji wa bidhaa.