Wakazi wa kaunti ya Kwale wametakiwa kutofuata kauli ya vuguvugu la MRC la kuwakataza wananchi kutopiga kura.

Wachumba wawili wanaodaiwa kuhusika kwa ulanguzi wa watoto watasalia korokoroni kwa muda wa wiki mbili wakisubiri uchunguzi kukamilika dhidi yao.

Upungufu wa vituo vya kurekebisha tabia waathiriwa wa mihadarati nchini ni changamato kuu katika juhudi za kukabiliana na utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa waathiriwa hao.

Mtaii mmoja huko Malindi amevamiwa na watu wasiojulikana  na  kumsababishia majeraha mwilini.

Katibu katika wizara ya uchukuzi Irungu Nyakera amewatoa hofu wakenya kuhusu kuporomoka kwa mchanga kwa sehemu ya reli ya kisasa inayoendela kujengwa eneo la Makueni.

Waziri wa elimu Dkt Fred Matiangi amekamilisha ziara yake kaunti ya Kwale kwa kutembelea shule kadhaa za msingi za eneo hilo mapema leo kutathmini hali na jinsi mtihani wa kitaifa wa darasa la nane unavyosimamiwa.

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Moi anayekabiliwa na madai ya ugaidi atazuiliwa  korokoroni kwa muda wa siku 10 kusubiri uchunguzi kukamilika.

Mabalozi wa nyumba kumi huenda wakapata sababu ya kujitolea zaidi katika kazi yao hiyo inayohatarisha maisha baada ya serikali kusema itaanza kuwapa marupurupu.

Mwenyekiti wa baraza la kitaifa la ushauri kwa waislamu nchini KEMNAC Sheikh Juma Ngao amewatahadharisha waislamu dhidi ya kundi moja la watu lililochipuka analolitaja kama lenye nia ya kuzuia jopo liloteulia kufanyia marekebisho sheria za wakfu wa waislamu kutofanya kazi zake.

Polisi waliomuua Kwekwe Mwandaza wamekata rufaa katika mahakama ya Mombasa kupinga kifungo cha  miaka 7 walichopewa.

Hatimaye mbunge wa Matuga Hassan Mwanyoha ametoa kauli yake kuhusu hukumu ya kifo aliyopewa mwanawe Mafanikio Hassan Mwanyoha almaarufu  Fani Hussein  Hassan na mahakama ya Kwale wiki iliyopita kwa kumpata na hatia ya wizi wa mabavu.

Familia ya Mwalachu huko Ukunda kaunti ya Kwale inaomboleza kifo cha nduguyao Hamisi Mwalachu aliyetekwa nyara na mwili wake kupatikana umetupwa katika msitu wa Voi kaunti ya Taita Taveta hapo jana.

Imebainika kuwa msichana mwenye umri wa miaka 10 aliyefariki wakati alipotaka huduma za kujifungua katika zahanati ya Ganze ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi ya Mtsanganyiko. 

Huku joto la kisiasa la uchaguzi mkuu ujao likiwa limeanza,viongozi mbalimbali wa kidini wameweka mikakati ya kuhakikisha kuwa amani na usalama unadumishwa hapa pwani.

Mtoto wa miaka miwili amepoteza maisha yake huku mwenzake akiponea baada ya nyumba yao kuteketea moto usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kongowea.