Sheikh Ngao adai kuchipuka kwa kundi linalotaka kuzuia marekebishao ya sheria za Wakfu

Habari Zaidi
Typography

Ngao ambaye ni kamishna katika  wakfu huo  amesema kundi hilo linapanga kuelekea mahakamani kuzuia jopo hilo kufanya kazi yake ambapo lina jukumu ya kufanyia marekebisho sheria zinazosimamia wakfu huo pamoja na mali zote za wakfu huo.

Akizungumza na wanahabari hapa jijini Mombasa amedai kuwa kundi hilo tayari limeshapata huduma za wakili ambapo wanaendeleza mikakati ya kutaka kuzuia jopo hilo lililoteuliwa na rais.

Amesema kundi hilo linatumiwa na matajiri wanaofuja mali za wakfu ili kuzuia ukweli na haki kubainika.

Aidha ametishia kuwataja hadharani wale wote wanaohusika na harakati hizo hivi karibuni.

Ikumbukwe kuwa wakfu huo wa waislamu kwa muda umekumbwa na mzozo wa usimamizi kutokana na sheria za zamani hali iliyosababisha rais Uhuru Kenyatta kuunda jopo maalum kufanyia marekebisho sheria hizo.