Mabalozi wa nyumba kumi kuanza kupata posho

Habari Zaidi
Typography

Kwa mwaka watatu mabalozi wa nyumba kumi ambao ni jicho la serikali katika maswala ya usalama mitaani wamekuwa wakifanya kazi bure.

Katibu katika katika wizara ya usalama wa ndani Karanja Kibicho amesema serikali imetenga shilingi bilioni 1.2 ili kuwalipa marupurupu katika kila mkutano watakao hudhuria.

Aidha maesema kila mwezi watakua wakihudhuria mikutano isiyopungua miwili ambapo watapewa posho hiyo.

Kibicho ameyasema haya katika chuo cha mafunzo cha serikali hapa Mombasa, ambapo washikadau mbali mbali walikua wakipokea vyeti vyao baada ya kupokea mafunzo ya jinsi ya kuendesha shuhuli za serikali katika ngazi.