Mwanafunzi anayekabiliwa na madai ya ugaidi kusalia korokoroni

Habari Zaidi
Typography

Hassan kassim Hassan alitiwa mbaroni oktoba 31 na kuhusiswa na kundi la ISIS.

Hassan anadaiwa kutaka kusafiri hadi nchini Libya kujiunga na kundi la ISIS.

Hii ni baada ya afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kutaka kuzuiliwa mshukiwa huyo kwa muda wa siku 15 ili kufanyiwa uchunguzi.

Mwendesha mashtaka Eugine Wangila alisema mshukiwa huyo huenda atatoroka iwapo ataachiliwa.

Jambo lililopingwa na Wakili wa mshukiwa Mohammed Fakii, kwa kusema mteja wake hawezi kutoroka.