25
Sun, Feb

Sehemu ya barabara ya reli ya kisasa yaporomoka

Habari Zaidi
Typography

Nyakera ameeleza kwamba sehemu hiyo ilikuwa bado inajengwa ndio mvua ikanyesha na kufanya sehemu hiyo kuporomoka na hilo ni jambo la kawaida katika ujenzi ambao haujakamilika.

Katika mitandao ya kijamii Facebook, Twitter na Watsup watu wengi wameishutumu kampuni ya Uchina inayotengeza barabara hiyo wakisema reli hiyo inaogopesha iwapo inaweza kuporomoka wakati haijaanza kufanya kazi.

Mradi wa reli ya kisasa unanuai kuunganisha Kenya na mataifa jirani ambapo itakuwa na urefu wa kilomita 609.

Wengi wamehusisha kuharibika kwa reli hiyo na ufisadi unaoendelea nchini.

Katika Twitter wengi wametilia shaka uthabiti wa reli hiyo ambayo imeshindwa kuhimili mvua chache.