25
Sun, Feb

Mtalii ashambuliwa huko Malindi

Habari Zaidi
Typography

Kulingana na wahudumu wa pikipiki waliozungumza na mwanahabari wetu, kisa hicho kimetokea sehemu ya barabara inayoelekea Casuarina.

Wamesema mhasiriwa amekatwa kwa panga kabla ya kuokolewa na kukimbizwa katika hospitali kuu ya kaunti ndogo ya Malindi kwa matibabu.

Afisa mkuu wa upelelezi kaunti ndogo ya Malindi Paul Wachira amesema mtalii huyo hayuko katika hatari yoyote kwani ametibwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.