25
Sun, Feb

Uhaba wa "Rehab Centres" changamoto kukabili janga la mihadarati

Habari Zaidi
Typography

Haya ni kulingana na hakimu wa mahakama ndogo ya Lamu Njeri  Thuku.

Aliyekuwa akizungumza  katika warsha iliyoandaliwa na idara ya mahakama ili kuwafahamisha wananchi wa kaunti ya Lamu juu ya utendekazi wa idara hiyo katika uwanja wa Mkunguni kisiwani Amu.

Thuku amesema kisheria serikali kuu inafaa kuwa na vituo hivyo ambavyo watumizi wa mihadarati wanapohukumiwa na mahakama  wanafaa kupelekwa badala ya kupelekewa katika jela za kawaida kama inavyofanyika kwa sasa.

Thuku amesema iko haja ya vituo hivyo kujengwa huku akitoa wito kwa serikali kuu na wafadhili kujenga vituo hivyo kwa ajili ya kusaidia waathiriwa wa mihadarati katika jamii.