25
Sun, Feb

Washukiwa wa ulanguzi wa watoto kusalia Korokoroni

Habari Zaidi
Typography

Margaret Juma Magero na David Ochieng Ometo wanadaiwa kuhusika katika ulanguzi wa watoto watatu.

Machi 18 mwaka 2009, wanadaiwa kuiba  Breluin Achieng mwenye umri wa miaka saba ambaye ni mtoto wa Lilian Akinyi Ongwane katika mtaa wa  Maweni eneo la Kisauni.

April 4 mwaka 2011 wanadaiwa kuiba , Joyce Mbuche mwenye miaka mitano ambaye ni mtoto wa Sidi Mwamumbo Chaga katika eneo la Bamburi.

Pia wanadaiwa kuiba mtoto kwa jina Baby Brian mwenye umri wa mwaka mmoja unusu ambaye hajafahamika wazazi wake halali.

Wawili hao wamefikishwa katika mahakama ya Shanzu mbele ya hakimu Diana Mochache.