25
Sun, Feb

Wakazi wa Kwale watakiwa kutofuata kundi la MRC

Habari Zaidi
Typography

Wakazi hao wametakiwa kujiandikisha kwa wingi kama wapiga kura ili kuchaguwa viongozi wenye kuleta maendeleo.

Kauli hii imetolewa na mwakilishi wa wadi ya Kinondo huko Msambweni Juma Maone.

Maone amesema kuwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo wametishiwa maish na wafuasi wa MRC, dhidi ya kujiandikisha kama wapiga kura.

Amewataka wakazi hao kutokubali kutishiwa na kundi hilo ambalo linadai kujitenga kwa sehemu ya Pwani.

Ameongeza kuwa Pwani bado ni Kenya na haiwezi kamwe kujitenga.

Kauli yake imeungwa mkono na mwakilishi wa wadi ya Tiwi, Omar Mwakwambirizwa, aliyewataka vijana kutokubali kutumiwa na kundi hilo ambalo amelitaja kupoteza mwelekeo.