25
Sun, Feb

Inspekta wa polisi nchini akosa kumfikisha katika mahakama ya Milimani Miguna Miguna.

Habari Zaidi
Typography

Jaji wa mahakama kuu Luka Kimaru amemuagiza mkurugenzi wa mashitaka ya umma kufika mbele yake leo saa sita mchana kuelezea iwapo mwanasiasa Miguna Miguna ameshitakiwa au la. 

Hii ni baada ya kiongozi wa mashtaka Nicholas Mutuku kumwambia jaji Kimaru kwamba Miguna amefikishwa mapema leo katika mahakama ya Kajiado badala ya Milimani kama ilivyoagizwa jana. 

Jaji Kimaru pia ameahidi kutoa uamuzi wake iwapo Inspekta generali wa polisi Joseph Boinett na George Kinoti wamekiuka agizo la mahakama baadaye mchana wa leo.

Ikumbukwe kuwa hapo jana jaji Kimaru aliagiza inspekta mkuu wa polisi na mkuu wa idara ya upelelezi kufika mahakamani na kumwasilisha Miguna Miguna hii leo.

Hata hivyo wawili hao wametuma wawakilishi wao

Hata hivyo naibu mkurugenzi wa mashtaka ya umma  amesema ,mapema leo Miguna amefikishwa katika mahakama ya Kajiado na haina haja ya inspekta mkuu na mkuu wa idara ya upelelezi nchini kuchukuliwa kwamba wamekiuka agizo la mahakama.

Hata hivyo mawakili wa Miguna wanataka mteja wao awasilishwe katika mahakama ya Milimani jijini Nairobi.

Miguna ambaye anajiita generali wa kundi la NRM alikamatwa siku ya ijumaa nyumbani kwake Runda Jijini Nairobi na amekua akizuiliwa na polisi tangu siku hiyo licha ya mahakama kuamuru aachiliwe kwa dhamana ya shilingi elfu 50.