25
Sun, Feb

Wazazi watishia kuandamana kushinikiza kuondolewa kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Majengo-Kasemeni.

Habari Zaidi
Typography

Wazazi  wa shule ya msingi ya Majengo huko Kasemeni eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale wametishia kuandamana kushinikiza  kuondolewa kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo kwa madai kuwa anawadhulumu wanafunzi.

Hii  ni baada ya wanafunzi wawili kukosa kufanya mtihani wa K.C.P.E mwaka jana licha ya kulipishwa shilingi 200 kila mmoja wao kama ada ya mtihani huo. 

Akizungumza na vyombo vya habari mzazi  Nyamawi Mangale Mwatengele amesema wanawe Kajumwa Mangale na Nyamvula Mangale walikosa kukalia mtihani huo baada ya mkuu wa shule kudai baraza la kitaifa la mitihani lilifutilia mbali majina yao jambo ambalo wazazi hao wanasema kuwa sila ukweli.

Juhudi za mwanahabari wetu kupata kauli ya mwalimu mkuu wa shule hiyo kuhusiana na swala hilo hazikufua dafu.

Hata hivyo mkurugenzi wa elimu kaunti ya Kwale Bridgit Wambua amewashauri wazazi kutafuta  mwafaka wa kusuluhisha tofauti zao na walimu badala ya kuandamana.