25
Sun, Feb

Ukosefu wa usalama wapelekea kuvunjwa kwa vibanda vya biashara Malindi.

Habari Zaidi
Typography

Kamati ya usalama huko Malindi imesema changamoto ya usalama ndio ilipelekea maafisa wa polisi na askari wa kaunti ya Kilifi kubomoa vibanda vya wafanyibiashara hapo jana katika eneo la Kwa Baya.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Karung'o Kamau amewaambia waathiriwa kwamba eneo hilo limezingirwa na kuwa sasa ni maficho ya mateja ambao wamekuwa tishio kubwa la usalama kwa wananchi.

Eneo hilo ambalo limekuwa machoni mwa maafisa wa polisi na limekuwa likivamiwa kila mara na polisi wakiwasaka walanguzi, limeanza kuwa tishio kwani inaarifiwa mateja hao wamekuwa wakiwavamia wapita njia na kuwaibia.

Lakini wafanyibiashara hao wamewalaumu polisi kwani wamekuwa wakiwakamata mateja hao na kisha kuwawachiliwa.

Hata hivyo wafanyibiashara hao wametishia kuchukua sheria mikononi mwao na kuwafurusha mateja hao iwapo polisi watashindwa kuwakabili wakisema mateja hao wameharibu biashara yao.