Viongozi wa nchi za IGAD wakutana mara ya kwanza Mogadishu

Africa
Typography

Imekuwa mara ya kwanza kwa mkutano kama huo kufanyika mjini Mogadishu tangu kuanzishwa kwa muungano huo miaka 30 iliyopita.

Viongozi kutoka Kenya, Uganda , Ethiopia na Somalia walihudhuria mkutano huo.

Wakati wa mazungumzo yao, viongozi hao walitoa hakikisho kuwa jamii ya kimataifa na washirika wako tayari kuisadia Somalia, kuhakikisha kuwa uchaguzi umefanyika wakati ufaao kuambatana na matakwa wa watu wa Somalia.

Pia suala la kurejeshwa kwa wakimbizi wa Somalia kutoka nchini Kenya ambalo limekuwa likiendelea kwa miaka mitatu sasa. Viongozi hao sasa wametoa wito wa kutaka kufanyika zoezi hilo kwa njia ya amani.

Adha serikali ya Somalia ilitangaza kuwa imeondoa marufuku ya usafirishaji wa miara kutoka nchini Kenya. Marufuku hiyo ilitangazwa wiki moja iliyopita na imesababisa hasara ya mamilioni ya dola kwa wakulima wa miraa nchini Kenya.

Wengi wa wanachama, Ethiopia, Uganda na Kenya, wamechangia wanajeshi katika kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika ambacho kinasaidia serikali kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu wa al-Shabab.

Source: BBC