25
Sun, Feb

Robert Mugabe atimiza umri wa miaka 93

Kimataifa
Typography

Mugabe ambaye ndiye kiongozi wa taifa mkongwe zaidi duniani atasherehekea siku yake ya kuzaliwa mjini Harare.

Hata hivyo sherehe kubwa inatarajiwa kuandaliwa siku ya Jumamosi katika mbuga ya wanyama pori ya Matobo nje ya mji wa Bulawayo ambako maelfu ya wafuasi wa chama tawala cha ZANU PF na maafisa wa serikali wanatarajiwa kuhudhuria.

Sherehe hiyo inatarajiwa kugharimu zaidi ya Dola milioni mbiliMugabe amesema hana nia ya kuondoka madarakani akidai maafisa wa chama chake hawajapata mtu anayestahili kuchukua madaraka kutoka kwake.

Mugabe amesema maafisa wa ZANU PF wanamtaka agombee tena urais 2018, na kuongeza iwapo atahisi hawezi tena, atakieleza chama chake lakini kwa sasa hadhani kama muda wa kuchia madaraka umefika.

COURTESY DW/SWAHILI