25
Sun, Feb

Wachimba mgodi waliokwama watolewa salama salimini huko Afrika Kusini

Kimataifa
Typography

Wachimba migodi wote 995 waliokuwa wamenaswa chini ya mgodi kutokana na kukatika kwa nishati ya umeme wametolewa salama salmini. 

Taarifa hiyo imetolewa na mmiliki wa mgodi wa Sibanye Gold nchini Afrika Kusini. 

Msemaji wa kampuni hiyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba hapakuwapo na tukio lolote la kutisha ukiacha tu mikasa kwa baadhi ya wafanyakazi hao kukaukiwa maji mwilini na kubanwa na shinikizo la damu. 

Wachimba mgodi hao walinaswa chini ya mgodi kwa muda wa karibu saa 30 katika mji mdogo wa Theunissen ulioko katika jimbo la Free State, Afrika Kusini. 

Waliweza kuokolewa baada ya juhudi zilizochukua muda wa saa mbili ambapo nishati ilirejeshwa na hivyo kuweza kuwapandisha juu watu hao.

KWA HISANI YA DW