25
Sun, Feb

Karani adai nyoka alikula mamilioni ya pesa Nigeria.

Kimataifa
Typography

Karani mmoja nchini Nigeria amefukuzwa kazi baada ya kuwaambia wakaguzi wa hesabu kuwa nyoka alikula naira milioni 36.

Pesa hizo ni sawa na dola 100,000 za kimarekani.

Karani Philomena Chieshe alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya bodi ya mtihani ya Nigeria inayokusanya pesa za mtihani.

Bodi hiyo ya mtihania iliiambia BBC kuwa ilitupilia mbali madai yake na imeanzisha kumchukulia hatua za kinidhamu.,

Kisa hicho kimezua shutuma na dhihaka kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria.

KWA HISANI YA BBC SWAHILI.