Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanya majaribio ya mtambo wake mpya, ambao unaweza kurusha makombora kutoka bara moja hadi jiingine, katika juhudi za kuimarisha uwezo wake wa kufanya mashambulio dhidi ya Marekani.

Siku moja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la haidrojeni, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana kuanza mikakati ya kuiwekea vikwazo.

Maafisa wa Afghanistan wanasema kuwa wamedhibiti maeneo muhimu ya mji wa kaskazini wa Kunduz kutoka kwa wapiganaji wa Taliban.

Takriban watu 140 wameuawa baada ya ndege ya uchukuzi wa kijeshi ya Indonesia kuanguka jana katika maeneo yenye makazi ya watu huko Medan Sumatra.

Habari kutoka kwa serikali ya Afghanistan zimeiambia BBC kuwa kinara mkuu wa kundi la wapiganaji wa Taliban, Mullah Omar amefariki.

More Articles...